PhotosSee All
'Mataifa yaliyostawi kiuchumi yamehimizwa kushirikiana na mataifa yanayoendelea ili kuwezesha utekelezaji wa Agenda ya Maendeleo ya mwaka 2030. Hayo ni kwa mujibu wa wajumbe wanaohudhuria kongamano la pili la ngazi ya juu kuhusu Ushirikiano wa Kimaendeleo Ulimwenguni linalofanyika mjini Nairobi.'
'Baada ya mamia kwa maelfu ya watu kuhudhuria Misa ya Wafu kwa ajili ya mwanamapinduzi wa Cuba, Fidel Castro, majivu ya kiongozi huyo wa zamani yanaanza kusafirishwa kutoka mji mkuu Havana hadi mjini Santiago kwa ajili ya mazishi hapo Jumapili, umbali wa kilomita 900. Mchora katuni wetu, @[104471662929072:274:GADO] Mwampembwa, anamuaga Fidel kwa mchoro huu.'
'Wanachama wa shirika linalosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC wamefikia makubaliano ya kuwekea kikomo uchimbaji wa mafuta-kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.Duru za OPEC zimeliambia shirika la habari la Reuters.Kabla ya hapo wanaachama wa shirika la ubia la OPEC walitoa dalili za hali hiyo kufuatia majadiliano ya kina mjini Vienna.'
VideosSee All
Papo kwa Papo 29.11.2016
1.6K
61
Kenya yapania kuongeza thamani ya kahawa yake ili kuimarisha k...
278
48
Papo kwa Papo. 19.11.2016
367
55
PostsSee All

Mashabiki wa klabu ya Chapecoense ya nchini Brazil wakusanyika kwa maombolezo. Raia wa Cuba wanaomboleza kifo cha kiongozi wao Fidel Castro. Na Bunge la Korea Kusini linatarajiwa kupiga kura ya kumshitaki rais wa nchi hiyo Park Geun-hye. Papo kwa Papo 30.11.2016

2.6K Views

Shirika la Afya Duniani-WHO limetoa mwongozo mpya wa watu kujipima wenyewe virusi vya HIV, siku moja kabla ya kuadhimishwa kwa Siku ya Ukimwi duniani.

463 Views
ReviewsSee All
1,529 Reviews
Tell people what you think
Shukuru Shuk
· November 28, 2016
A good radio station that we listen to in Africa and the whole world
Ahmed Bwire Elias
· November 18, 2016
Good luck on the way of this news
Posts

Mataifa yaliyostawi kiuchumi yamehimizwa kushirikiana na mataifa yanayoendelea ili kuwezesha utekelezaji wa Agenda ya Maendeleo ya mwaka 2030. Hayo ni kwa mujibu wa wajumbe wanaohudhuria kongamano la pili la ngazi ya juu kuhusu Ushirikiano wa Kimaendeleo Ulimwenguni linalofanyika mjini Nairobi.

Image may contain: skyscraper, sky and outdoor

Baada ya mamia kwa maelfu ya watu kuhudhuria Misa ya Wafu kwa ajili ya mwanamapinduzi wa Cuba, Fidel Castro, majivu ya kiongozi huyo wa zamani yanaanza kusafirishwa kutoka mji mkuu Havana hadi mjini Santiago kwa ajili ya mazishi hapo Jumapili, umbali wa kilomita 900. Mchora katuni wetu, GADO Mwampembwa, anamuaga Fidel kwa mchoro huu.

No automatic alt text available.

Wanachama wa shirika linalosafirisha mafuta kwa wingi duniani OPEC wamefikia makubaliano ya kuwekea kikomo uchimbaji wa mafuta-kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008.Duru za OPEC zimeliambia shirika la habari la Reuters.Kabla ya hapo wanaachama wa shirika la ubia la OPEC walitoa dalili za hali hiyo kufuatia majadiliano ya kina mjini Vienna.

No automatic alt text available.

Shirika la afya duniani WHO limetoa miongozo mipya kuhusiana na upimaji wa virusi vya HIV kutekelezwa na watu binafsi ili kuboresha huduma ya upimaji wa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi. http://bit.ly/2gUVXGa

Shirika la afya duniani WHO limetoa miongozo mipya kuhusiana na upimaji wa virusi vya HIV kutekelezwa na watu binafsi ili kuboresha huduma ya upimaji wa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa ukimwi.
dw.com|By Deutsche Welle (www.dw.com)

Rais wa Tanzania John Magufuli ameibatilisha hati miliki ya kipande kikubwa cha shamba la aliyekuwa waziri mkuu Fredrick Sumaye kwa sababu halikuwa limeendelezwa. Sumaye naye anasema hatua hiyo imechochewa kisiasa. Miezi michache iliyopita serikali ilianzisha operesheni ya kutwaa ardhi ambayo haijaendelezwa na wawekezaji na kuirejesha kwa wakulima maskini.

Image may contain: one or more people

Kwa mara ya kwanza kwa miaka 22 iliyopita baada ya mauaji ya halaiki, Rwanda imetangaza kuwashitaki mahakamani wafaransa 20 wanaoshutumiwa na Rwanda kuhusika kwenye mauaji hayo. Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Rwanda amesema,idadi hii inaweza kuongezeka lakini upelelezi wa awali unaonyesha watu hao 20 ndiyo watakaofunguliwa mashtaka na Rwanda.

No automatic alt text available.

Ungana na Bruce Amani na Isaac Gamba muda mfupi ujao kweye Dunia Yetu Leo Mchana moja kwa moja kutoka studio za Idhaa ya Kiswahili ya DW hapa Bonn.

Posted by DW (Kiswahili)
1,090 Views
1K Views

Mfalme wa kimila nchini Uganda Jumanne hii amefunguliwa mashitaka ya mauaji na kupelekwa kwenye kizuizi chenye ulinzi mkali, taarifa kutoka kwa afisa wa serikali zimesema. Hatua hii inafuatia makabiliano kati ya walinzi wa mfalme huyo na jeshi ambayo yalisababisha vifo vya kiasi ya watu 62.

Image may contain: 1 person , suit

Mkutano wa asasi za kupambana na kuzuia rushwa Afrika Mashariki umefanyika Tanzania. Washiriki wanataka kufuatilia uhalifu na kuweka mkakati wa kurejesha fedha zinazotoroshwa na kufichwa nje ya nchi. Je, ni katika mazingira yapi bado unakutana na utoaji na upokeaji rushwa?

dw.com|By Deutsche Welle (www.dw.com)

Je utakubali kufanyiwa upasuaji wa kuziba mshipa wa kupitisha mbegu za kiume kama njia ya kupanga uzazi? Ikiwa wewe ni mwanamke je utamshauri mpenzi wako au mume wako atumie mbinu hiyo ya upangaji uzazi? Sababu zako ni zipi? Sikiliza makala kisha utupe fikra yako.

Ni kwa nini wanaume wengi huchelea kushiriki mbinu za upangaji uzazi zinazohusu upasuaji? John Juma anazungumza na wahusika kwenye makala ya Afya Yako
dw.com|By Deutsche Welle (www.dw.com)

Mara ya mwisho wewe kusoma kitabu ilikuwa lini na ulisoma kitabu gani? Tuambie kwanini unapenda kusoma, na kama hupendi vile vile tufahamishe.

Je kusoma kama uraibu kumeendelea kwa kiwango gani barani Afrika? Dhana kuwa waafrika husoma tu ili wafaulu mitihani ni kweli? John Juma anakupa mitizamo katika makala ya Utamaduni na Sanaa, ya Idhaa ya DW -Kiswahili
dw.com|By Deutsche Welle (www.dw.com)

Kasheshe limendelea mjini Kasese Magharibi mwa Uganda, baada ya mapigano kati ya vikosi vya usalama kuuwa watu 62, wakiwemo maafisa 16 wa polisi. Mfalme wa Rwenzururu Wesley Mumbere ambaye walinzi wake walipambana na jeshi, tayari kawekwa kizuizini na silaha nyingi zimekamatwa. Ni Papo kwa Papo.

5.2K Views

Yusra Buwayhid ndiye atakuwa nahodha wako kuliongoza jahazi la matangazo ya jioni ya DW tangu mwanzo mpaka mwisho. Miongoni mwa mada zetu:
- Afrika Kusini: Chama tawala cha ANC kimekataa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma na hivyo hatalazimika kujiuzulu, licha ya kukumbwa na kashfa za rushwa.
- Chama cha Fatah cha Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, kimeanza mkutano wake mkuu hii leo. Abbas mwenye miaka 81 amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa chama.
- Watu 149 wamekamatwa Uganda wakishutumiwa kuhusika na mapigano kati ya wanamgambo na maafisa wa usalama yaliyoua watu 62.
Jiunge nasi kupitia redio yako au kupitia dw.com/kiswahili.

Image may contain: 1 person , screen

Mshauri mkuu wa rais wa Burundi anusurika jaribio la kuuawa. Ndege iliyobeba wachezaji yaanguka Colombia na kuua watu 75. Vikosi vya Syria vyakomboa thuluthi ya Mashariki ya Aleppo. Ban Ki-moon ashutumu ghasia na mauaji katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Papo kwa Papo 29.11.2016

10K Views
Tunakuletea yaliyomuhimu. Unatupa fikra yako: Jadiliana nasi habari kutoka Afrika na ulimwengu mzima.
Visitor Posts
People Also Like
Liked by This Page
PlacesBonn, GermanyDW (Kiswahili)