Photos
Videos
Uwe na Jumapili nzuri msomaji wetu wa Tizneez. Kitu pekee ambacho unapaswa kuwa nacho wakati wote ni Furaha. Furahia maisha yako kwa maana hakuna mengine baada ya hapa. Maana kitu kizuri katika maisha ni maisha yenyewe, Hivyo ni vyema kuwa ndani ya furaha lakini furaha iwe ndani yako. Jumapili ikawe njema kwako. #TuzungumzeMuziki cc @legendeeofficial @johmakinitz www.tizneez.com
1
Nyakati zote waswahili husema "Usiwashe taa nyumbani mwa kipofu" Msemo huo/huu una maana kubwa na yenye uhalisia wa muziki wetu sasa. Tupo kwenye kizazi ambacho katika ile kweli hakijui thamani ya kipaji lakini thamani ya muziki wenye maana na uzuri. Wengi wamesimamia matendo ambayo hayana uhusiano wowote na muziki.(Fedheha) Lakini mashabiki hupenda zaidi watu wazungumze habari hizo. (Ujinga) Wengine husema kwanini Tizneez mnasifu hata mrudio wa wimbo? lakini yafaa mjue twasifu maana yafaa tusifu, kwa kitu bora kilichofanywa na mhusika. Ni wazi @dreammswazi umefanya kitu kikubwa na kizuri hatuna budi kufungua vinywa vyetu na kusema hadharani maana yafaa tuhubiri kweli wakati wote. Lakini kaka yetu tunakumbusha tu "Usisahau ubaharia shauri ya unahodha" Ni vyema kusimamia vyema kwenye muziki. #TuzungumzeMuziki www.tizneez.com
7
1
@nikkimbishi msanii bora wa sasa katika mambo matatu Midondoko, Uandishi, na Kujiamini. Lakini shauri ya ukanda, urafiki, undugu kutoka kwa watu wa Media unafanya kukosa nafasi ya Watanzania walio wengi kujua thamani kubwa ya msanii huyu. Kama kweli ingekuwa inatazamwa muziki wa mtu na sio kitu kingine kwa hakika Nikki Mbishi ni bora kuliko wengi mno wavumao kwenye upepo wa upande mmoja (Media) Ni wazi ni Nikki ni alama bora na kubwa kwenye muziki wa hiphop kwa sasa. www.tizneez.com Link kwenye bio juu.
4
Posts

#TuzungumzeMuziki
Kati ya hizi za @roma_zimbabwe Ni ipi kwako ni bora wakati wote?
1. Tanzania

2. Viva Roma Viva Feat Chibwa ...
3. 2030

4. Mr President

5. Mathematics

6. Mechi za Ugenini Feat Jose Mtambo

7. Zimbabwe

8.KKK

9. Pastor

10. Kaa Tayari Feat Darassa & Jose Mtambo.

Tuambie ipi ni bora wakati wote?

See More
Image may contain: one or more people, people on stage, crowd, sky, night and outdoor

#TuzungumzeMistari "Misiba imepoteza uchungu, harusi zimepoteza shangwe"

Bonta aliyaona na kuyasema haya kwenye wimbo wa Tukutane Maktaba miaka kadhaa iliyopita.

Sasa mnashangazwa na nini katika maisha ya leo hii?

...

Kizazi hiki cha mtandao kitachukua muda mno kumuelewa Bonta.

Maana nguvu kubwa ya Media ni kupromote muziki ambao wao huita mzuri, sasa sijui muziki mbaya ni upi!

Au ni huu wa kuelimisha jamii na kujenga akili za watu ndiyo muziki mbaya?

Hakika "Mwenye moja havai mbili" (Chukizo)

#TuzungumzeMuziki

See More
Image may contain: one or more people
Posts

Picha ikimuonesha Chid Benz na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh Paul Makonda.

Wengi wamekuwa wakifurahia jambo la Chid Benz kuwa kwenye mikono ya Mh Paul Makonda kwa maana ya kuona yakuwa sasa atakwenda kusaidiwa kutoka katika tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya.

Lakini msanii mkongwe wa HBC kaka yetu Fanani ambaye aliwahi kuzama katika dimbwi la matumizi ya madawa ya kulevya aliwahi kutuambia "Mtu hawezi kuachishwa matumizi ya madawa,bali yeye mwenyewe kuacha"

...

Lakini tukirejea semi ya mswahili inayosema yakuwa " Kila mlango na funguo yake"

Inatupa maana ya kuwaza vyema juu ya Chid Benz kwa upana wa yeye ndiye mwenye funguo ya mlango wake wa maisha.

Hakuwa awezae kufungua mlango wake,bali wengi wataishia kuuchokonoa na kuushindwa.

Hivyo maamuzi ya muda gani afungue mlango wake anayo yeye katika viganja vyake lakini ufahamu wake.

Sisi wengine hata tupaze sauti vipi ni wazi ataona ni watu ambao hatumtakii mema maana alipozama yeye anapaona pema kwa macho yake ya ndani kabisa.

Lakini waswahili husema "Kwenye wengi hapaharibiki neno"

Ila yafaa mjue yakuwa "Kilichoma baharini, kakingoje ufukoni"

#TuzungumzeMuziki

www.tizneez.com soma zaidi link kwenye bio juu.

See More
Image may contain: 3 people

@daynanyange alipata mtoto akiwa chini ya miaka 18.

Na sasa mwanae ana miaka 11, lakini licha ya yote Dayna hakuweza kupata elimu ya Sekondari bali msingi.

Ila nyakati zote za sasa anapigana vyema mwanae aweze kufika mbali kielemu.

...

Na tukitazama muziki si rasmi maana hata sera ya nchi haipiganii wala haitambui muziki huu.

Licha ya porojo nyingi mno kuwepo. Leo Dayna anampeleka mwanae shule nzuri ambayo yeye anaamini kana kwamba mwanzo wake ungelikuwa mzuri ni wazi angelifika mbali.

Hivyo amemuanzishia mwanae msingi mzuri ili nyumba yake ya elimu iwe njema baadae.

Hivyo kama muziki wetu ungetazamwa kwa jicho la kwanza ni wazi ungekuwa sehemu ya kuokoa maisha ya watu wengi mno.

Na ikumbukwe tukisema mafanikio hatupaswi kutazama mtu mmoja au wawili bali katika wengi wenye daraja sawa la mafanikio.

Amani kwako wewe ambaye hukuweza kupata elimu ya darasani lakini umefaulu elimu ya maisha.

Kwa kutumia kipaji chako na kuamini yakuwa inawezekana bila ya elimu ya darasani.

#TuzungumzeMuziki cc @daynanyange
www.tizneez.com link kwenye bio juu.

See More
Image may contain: 1 person

#TuzungumzeMuziki

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha Ea Radio, msanii wa muziki wa bongo fleva Bonge la Nyau anasema yakuwa "Kutengeneza hits song ni kipaji"

Hivi ni kweli kutengeneza hits song ni kipaji? au hutokea tu kama bahati?

...

Hebu tuambie uonavyo wewe shabiki.

See More
Image may contain: 1 person, sitting, shoes and outdoor
Tizneez shared a link.
21 hrs
Amber Lulu muimbaji mzuri ila mapito yake yanamgharimu. Waswahili hunena yakuwa "Usisahau ubaharia sababu ya unahodha" Ni vyema kusimama katika kweli ya ndani yako (Kipaji) na nyakati zote yafaa mjue yakuwa "Kawia ufike" Haraka ya kutaka jina kubwa kwa njia yoyote si njema, maana unaweza acha uhalis...
tizneez.com

#TizneezThrobackMusic
Moja ya Album bora kuwahi kutokea kwenye muziki wa kizazi kipya ni Mwanafalsafani ya @mwanafa
Hakika Album hii ni bora nyakati zote za maisha ya muziki huu.

Mwanafalsafani ni album ambayo ilitoka mwaka 2002.

...

Na nyimbo ambazo zinapatikana kwenye album hii ni

1. Ingekuwa vipi Feat @jaymoefamous
2. Sitoamka Feat @jidejaydee
3. Upanga Feat @aytanzania @kingcrazy_gk @adam_snare & Kasiri

4. Mabinti

5. Sala

6. Show Time

7. Unanisikiza Mchumba

8. Haturap Remix Feat Kasiri & Jlt.

Ni wazi nyakati hizo bila uwezo wa kimuziki huwezi kuchomoza maana muziki ulikuwa muziki na mashabiki walizingatia muziki.

@mwanafa Moja ya wasanii ambao wanapaswa kuheshimiwa kwa wakati wote katika huu muziki kwa maana kuwa na mchango mkubwa wa kukuza na kueneza muziki huu ambao sasa ni ajira ya wengi.

#TuzungumzeMuziki

See More
Image may contain: 1 person, text

Hanscana Ataja kazi ambayo angefanya kama asingekuwa muongozaji Video.

Hanscana ni moja kati ya waongozaji video bora ambao tumebarikiwa kuwa nao kwenye uwanja wa muziki wa kizazi kipya.

Kupitia mtandao wa picha Instagram kwenye ukurasa wake Hanscana hakuacha kumjibu shabiki juu ya swali lake la "Kama usingekuwa muongozaji wa video ungefanya kazi gani?

...

Ambapo Hanscana amejibu kwa kusema "Ningelikuwa Daktari"

Hayo yamekuja baada ya Hanscana kuruhusu mashabiki wamuulize chochote mapema leo kwenye ukurasacwake wa mtandao wa picha 'Instagram'

#TuzungumzeMuziki
www.tizneez.com kusoma mengi zaidi.

See More
Image may contain: 2 people, people standing, sky, outdoor and nature

"Ukiwa huwezi kuwasaidia watu, angalau basi usiwaumize"
Hakika waswahili hawakukosea kunena yakuwa "Kuelewa nacho ni kipaji"

Tafakari... cc @niitesonga

Image may contain: 1 person

#TuzungumzeMuziki

Ukitafakari ukubwa wa @diamondplatnumz kwenye muziki ni wazi hutatamini ashuke bali apande kila leo.

Maana kupitia yeye tumeona wengi wakifaidika nyuma yake na hii inaleta maana ya sanaa ni kazi lakini inatoa kazi kwa watu wengine wenye kutaka kazi.

...

Kupambana kumshusha msanii huyu ni kushusha familia nyingi ambazo ziko nyuma yake.

Jambo jema ni kupambana kupandisha akina Diamond wengi ili sanaa iwe na uwanja mpana wa kutoa ajira nyingi kwa vijana wengi.

Hatupaswi tuwe wenye chuki na mafanikio ya msanii huyu bali kuwa wenye furaha.

Chuki za nini? na yafaa tupinge kwa upana msemo wa Lord Eyez wa Nako 2 Nako yakuwa "Yule yule atakakupandisha ndiye atakae kushusha"

Yafaa tusimamie semi za waswahili yakuwa "Aliyepandisha wengine ngazini, hupigwa teke menoni"

Hakika yafaa "Mdau apigwe teke menoni kama tu hathamini uwingi wa famalia nyingi nyuma ya msanii huyu"

www.tizneez.com link kwenye bio juu kusoma mengi.

See More
Image may contain: one or more people and people sitting

#TuzungumzeMuziki

Rapa @bill_nass amesema yakuwa hayupo chini ya Peti Money na sababu ya mtengano huo hajaziweka wazi maana yeye aliona taarifa mtandaoni kuwa Petii Money ameondoka"

Jambo hili kama msanii husika ameliona kwenye mtandao ina maanisha hawakuwa wakifanya kazi kwa makaratasi bali zile za ubro bro na udananda.

...

Tunarudia tena tukisema Muziki umekua yafaa walau twende na kasi na neno hilo kwa maana ya kutoa dosari zenye kubomoa muziki wetu.

Ni vyema @billnass kufahamu yakuwa "Anaekuja pasina hodi, huondoka pasina kuaga"

www.tizneez.com #TuzungumzeMuziki

See More
Image may contain: 1 person, smiling, sitting and shoes

#TuzungumzeMuziki
@richmavoko Ni moja kati ya wasanii wachache wenye uwezo wa kutunga na kuimba vyema.

Huwezi kutaja watunzi bora kwenye muziki wa kizazi kipya bila kutaja jina la Rich Mavoko.

...

Rich Mavoko ni Yeye na Muziki wake. Ikumbukwe wasanii wengi ni wasanii wa kuweka mbele mengi ambayo hayahusu muziki, lakini Mavoko ni yeye na muziki wake.

Licha ya wakati fulani kutaka kuingia katika dimbwi la kuzungumziwa nje ya muziki. (Lulu Diva)

Kwa Rich haikuwa na faida katika habari zake na kuonekana ni mwenye mahusiano na Lulu Diva.
Maana tangu kutoka kwake Rich hakuwahi kutanguliza mahusiano au jambo lolote nje ya muziki wake.

Na tunashukuru kwa kukumbuka yakuwa "Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu kwa kusimamia kile chenye maana katika biashara yake"

Na yafaa wakati wote @richmavoko ajue "Ukiwa tofauti pia itakufanya uonekane tofauti, hivyo ni vyema kuwa tofauti"

soma zaidi www.tizneez.com

See More
Image may contain: 1 person, sitting, shoes and sunglasses
Artist: Nikki Mbishi Tittle: Nimekumiss
tizneez.com

Tuhamie Mwezini Ya Dany Msimamo Feat Rama Dee & Suma G.

Ni wimbo bora wa wakati wote ambao umekosa nafasi kwenye uwanja wa Media.

Na hatuachi kusema yakuwa "Muziki mzuri haupo kwenye Media kwa maana ya Media hupiga nyimbo kwa nguvu ya ushawishi wa rushwa na sio ubora na ukubwa wa wimbo.

...

Amini tunawaambia ukweli ambao umesemwa kwenye wimbo huu ni ukweli ambao sasa unatokea katika maisha ya kila mmoja.

#TuzungumzeMuziki hakika huu ni wimbo bora katika vipengele vyenye kukamilisha upana wa wimbo bora.

Tungo, midondoko, na mdundo. Kuna wakati hutamani kusikia nyimbo za aina hii wakati mwingi zaidi ambazo zitajenga fikra na kuamsha mawazo ya wengi waliolala katika mengi yahusuyo maisha yao.

Na nyakati zote hatuachi kusema yakuwa "Kuna mengi yenye kushangaza kwenye muziki Kuna nyimbo za kila hisia, na kama ingetokea tunaishi kwenye ulimwengu usio na muziki hakika tungekuwa mahala pabaya"

Twasema tena Tuhamie Mwezini ni wimbo bora kwenye muziki huu ambao sasa umejaa tungo nyepesi na zenye vina lakini visivyo na maana.

Lakini nyakati zote waswahili hunena "Asali na shurubat hayana ladha moja"

#TuzungumzeMuziki

See More
Image may contain: night

King Zillah almarufu Godzillah ameweka maoni yake juu ya wimbo wa Mikono juu wa Nay wa Mitego kuwa ni wimbo mbaya.

Je!Ni kweli wimbo huu ni mbaya? #TuzungumzeMuziki

Image may contain: 1 person, sunglasses
Posted on: BATRO February 20, 2018 Music, Videos Comments WAKAZI – BAKORA (OFFICIAL MUSIC VIDEO) Post Views: 2 Tweet Share this on WhatsApp Papii Kocha – Waambie (Official Video) February 16, 2018 Comments Nikki Mbishi – Nimekumiss Official Video Comments Izzo Bizness – Saa Sita (Official Mu...
tizneez.com